current location : Lyricf.com
/
Songs
/
Mama lyrics
Mama lyrics
turnover time:2025-01-11 13:48:34
Mama lyrics

[Saida Karoli]

Oh garuko garuko garuke1

Oh garuke mwanawange2

Garuko garuko garuke

Oh garuke mwanawange

Ayee mbali ndi niyo wanyu3

Mbali ndi niyo wanyu

Mbali ndi niyo wanyu

Muda marefu umepita mwanangu

Tangu umefunga safari, iyeye

Urudi nyumbani uje uone hali yangu

Nakosa chumvi sukari, iyeye

Kila siku nakonda kufikiria sembe

Wapi ntapata mboga familia iende

Baba yako mgonjwa ashiki ata jembe

Toka '91 sina kipya kitenge

Iiih, noija noija maki mbwenu

Iiih, noija noija maki mbwenu

Kafukuzwa shuleni, mdogo wako Jane

Na mengine sisemi maiyoo

Sikai sebuleni nikiona wageni

Nakimbia madeni maiyoo

Iiih, noija noija maki baba

Iiih, noija noija maki mbwenu

Nitarudi mama, mama

(Taliwo akagenda akabura)4

Nitarudi mama, mama

(Taliwo akagenda akabura)

Nitarudi mama, mama

(Okebuke owanyu omuka)5

Nitarudi mama, mama

(Okebuke owanyu omuka)

Nitarudi mama, mama

[Rayvanny]

Heshima yako mama, ugua pole na baba

Mambo yatakuwa sawa, sipendi ukilalama

Kazi zimenijaa, na-hustle kupata chapaa

Nitakuja na pesa nyumbani, sahau kuhusu dagaa

Si unapendaga pete na chain nitaleta za gold

Mwambie mdogo wangu Jane ntampeleka boarding

Nitakujengea nyumba bondeni uache kulipa kodi

Ntakulipia yote madeni usigongewe hodi

Mwambie baba asijali

Atapona tutaenda hospitali

Asilie atakuwa shwari

Siku yake ya birthday nitampa gari

Machozi yanilenga

Siku zinakwenda mama

Sala zenu wapendwa

Ndo zitanijenga sana

Sijawatenga

Sikupigi kalenda mama

Mungu akipenda

Yote nitatenda mama

Naomba unisubiri nyumbani

Nitarudi mama, mama

(Taliwo akagenda akabura)

Nitarudi mama, mama

(Nitarudi ningojee)

Nitarudi mama, mama

(Okebuke owanyu omuka)

Nitarudi mama, mama

Nitarudi mama, mama

1. kwa Kiswahili: urudi2. kwa Kiswahili: urudi mwanangu3. kwa Kiswahili: nilipo ndipo kwenu4. kwa Kiswahili: safari siyo kifo5. kwa Kiswahili: pakumbuke nyumbani kwenu

Comments
Welcome to Lyricf comments! Please keep conversations courteous and on-topic. To fosterproductive and respectful conversations, you may see comments from our Community Managers.
Sign up to post
Sort by
Show More Comments
Rayvanny
  • country:Tanzania
  • Languages:Swahili, English, English (Nigerian Pidgin), Other, Portuguese
  • Wiki:https://en.wikipedia.org/wiki/Rayvanny
Rayvanny
Latest update
Copyright 2023-2025 - www.lyricf.com All Rights Reserved