current location : Lyricf.com
/
Songs
/
Diamond Platnumz - Zilipendwa
Diamond Platnumz - Zilipendwa
turnover time:2025-01-12 12:27:10
Diamond Platnumz - Zilipendwa

Oooh! hizo ni zama za kale

Oooh! Sangulo na pepe kalee,

Zilipendwa

[Rayvanny]

Eh! Kizamani, kutoa kadi na maua (zilipendwa)

Wanataka money ukilipa unakwarua (zilipendwa)

Ufundi kitandani, sio maguvu kujikamua (zilipendwa)

Unafika ndani, hujatomasa unachanua (zilipendwa)

Wanawake wa leo wanataka mikakati

Ukiwa mzugaji haki ya mungu huwapati (zilipendwa)

Mapenzi ya video yatakutoa kamasi

Eti nikinywa maji nakuona kwenye glasi (zilipendwa)

Eeh! kupiga chabo ghetto (zilipendwa)

Mkono na dettol (zilipendwa)

Sunche na Kapeto (zilipendwa)

Manjay na Mobeto (zilipendwa)

[Diamond]

Oooh! Hizo ni zama za kale

Oooh! Sangulo na Pepe kale

Mmm bolingo ndombolo (zilipendwa)

Twanga chipolopolo (zilipendwa)

Na maji ya kandoro (zilipendwa)

Simba wa Morogoro (zilipendwa)

[Rich Mavoko]

Tani sipati sukari guru kabisa (zilipendwa)

Hivi yuko wapi Mb Dogg wa Latiffa (zilipendwa)

Babu Tale wapi Papa Misifa (zilipendwa)

Siku hizi party hatuendagi Ibiza (zilipendwa)

Mpira na Pele (zilipendwa)

Tanu na Nyerere (zilipendwa)

Asha Ngedere (zilipendwa)

Arusi Mabele (zilipendwa)

Eti Uuze nyumba uweke heshima bar

Eti Ulazimishe aliyekukataa

Sabuni kicherema (zilipendwa)

Mabanda ya cinema (zilipendwa)

Lipumba na lema (zilipendwa)

Diamond na Wema (zilipendwa)

[Diamond]

Ooh hizo ni zama za kale (zama za zamani)

Ooh Sangulo na pepe kale (yoyoyo)

Mmm wakina soggy doggi (zilipendwa)

Chaneli analogy (zilipendwa)

Movie za saibogy (zilipendwa)

Van Dame, Arnoldi (zilipendwa)

[Queen Darleen]

Una nibeep nikupigie umeiweka vocha? (haloo)

Ule wewe nilipe mie umeniona lofa?

Tena na madada wenye majina acheni visa

Unaitwa ukale dinner mnakwenda Tisa

Nywele za kichina (zilipendwa)

Pochi za kuazima (zilipendwa)

Zena na Betina (zilipendwa)

Bashite Gwajima (zilipendwa)

[Diamond]

Ooh hizo ni zama za kale (zama za zamani)

Ooh Sangulo na pepe kale (yoyoyo)

Mmm Amita Bachani (zilipendwa)

Tv kwa jirani (zilipendwa)

Madee Rayvanny (zilipendwa)

Zari Ivanny (zilipendwa)

[Harmonize]

Yanini kunichunguza naishi wapi (zilipendwa)

Nala chapati kwa maini au makange (zilipendwa)

Kutwa kunikalia chini unakamati

Oh ya Rabi masikini kuni dhihaki

Ah sampamba pangala (zilipendwa)

P Funk Kajala (zilipendwa)

Onyango na Jangala (zilipendwa)

Rufufu mkandala (zilipendwa)

Vya nini vidomo domo tutupiane tunguli

Kisa pesa za mkopo msimu wa Magufuli

Ah, Bongoman yondo (zilipendwa)

Sikinde Msondo (zilipendwa)

Magari ya Udongo (zilipendwa)

Babu wa Loliondo (zilipendwa)

[Diamond]

Ooh hizo ni zama za kale (zilivumaga sana)

Ooh Sangulo na pepe kale (yoyoyo)

Ah Tv za kichogo (zilipendwa)

Wakina Man Dojo (zilipendwa)

Gigi na Iyobo (zilipendwa)

Akina Hatupogo (zilipendwa)

[Maromboso]

Eti msiba ukiona Bundi unataka kupagawa

Tulale makundi makundi kuogopa Popo Bawa

Zuwena nitampata wapi (zilipendwa)

Zuwena wa zile nyakati eh (zilipendwa)

Kujifanya mapanga zuna wamepinda

Wengine wabeba vyuma na hakuna marinda

Iddi Amini dada (zilipendwa)

Miuno ya H Baba (zilipendwa)

Domo Chai Jabba (zilipendwa)

Michezo ya kibaba baba (zilipendwa)

[Lava Lava]

Wale wapiga madeal sasa hali mbaya (zilipendwa)

Hizi zama za Magufuli si za Jakaya (zilipendwa)

Ugomvi wa Mr.Nice na Dudu Baya (zilipendwa)

Vikatuni vya madenge baba ubaya (zilipendwa)

Muhogo mchungu Mr. Bean, wapi bambo (zilipendwa)

Wale wazamiaji wale wa melini wazee wang'ambo

Hivi yuko wapi Benjamini wa Mambo Jambo

Wa Vietnam waporini vita na Rambo

Eh ndanda Mjela jela (zilipendwa)

Kidali Kombolela (zilipendwa)

Max na Zembwela (zilipendwa)

Juma Nature na fela (zilipendwa)

[Diamond]

Ooh hizo ni zama za kale (zama za zamani)

Ooh Sangulo na pepe kale (yoyoyo)

Mmm kamanda Daz Nunda (zilipendwa)

Kalumanzila Ndumba (zilipendwa)

Simu za Dole gumba (zilipendwa)

Johari na Kanumba (zilipendwa)

Wasafii

Zilipendwa, Zilipendwa

Zilipendwa, Zilipendwa

Ohlelelileleleleleee

Zilipendwa!

Comments
Welcome to Lyricf comments! Please keep conversations courteous and on-topic. To fosterproductive and respectful conversations, you may see comments from our Community Managers.
Sign up to post
Sort by
Show More Comments
Diamond Platnumz
  • country:Tanzania
  • Languages:Swahili, English, English (Nigerian Pidgin), Lingala
  • Genre:Folk
Diamond Platnumz
Latest update
Copyright 2023-2025 - www.lyricf.com All Rights Reserved