This is another one
Wengi wanakuombea utupu so piga kazi makini
Maana mtegemea cha ndugu heee utakufa maskini
Ndo maisha ya mjini changamoto mimi na wewe
Japo tulianza kuwa moto kabla ya moto wenyewe
Ndoto yangu ya milele sio tu kuimba na kuparty
Maaana mziki ni zaidi ya maisha kuvimba na magari
Bro, hili dili hatari fans kuja show shida
Wanasubiri ufe uweke rekodi ya kujarida
Sa mwelewe wazee mnapunga, pendeza wezeenu na nyumba
Ata sauti ina paa mzee ila huwezi kuwezeka nyumba
Huwezi kung'oa mchumba kama hauna doh mingi
Utaishia kujidunga bro maana stress ni mingi
Na mawazo kishimule, kichwani hauna shule
Dem wako anajiuza half na bei ni kama bure
Ndoto ukiwa nayo shule, hello ndugu na yaya tule
Walo kufa wote ni wajanja ndo maana wamewahi kule
Si since day one tupu zetu
Na wanaume waloshindwa kumpa mimba Wema Sepetu
Bigiri yechu yechu...
Shida, mwisho wa siku tunalia
U superstar mwiba, mzigo wa mwiba tunaubeba tunaumia
Mwanzo niliwaambia, ila kupitia haya mtakiri
Kujiongeza kwenye hakuna, tumizi mbaya la akili
Je hukubali kuuchuna huo upande wa pili
Wasikusemeshe ka mtu hajapiga mswaki wiki mbili
Namkiri ipo wazi hatuhifadhi makua
Kina sisi hatuna target tutoe wapi? Nafuu
Nipeni pasi ninyooshe miguu
Bwana mwane'nu nimejua kuwa dwanzi ndo ako ngazi za juu
Mara hiphop haiuzi asa hiphop ya juzi kina
Young Killer ndo mnaongoza kutoleta michuzi
Mara hiphop ime loosi ati hatuna ufumbuzi
Akina sisi hatuna Swagga sijui mpaka tufanyeje music
Huo ni uwongo na mnajua
Hakuna ashindwalo Mungu akitaka inakuwa
Dunia changamoto na maisha ni hatua
Alopitia tangu mtoto mpaka anakua
Mpaka anajua raha mechi kibao
Akipata kifua chumvi limao
Sa hivi Simba na anambao ndo hashindani
Ila Barcelona Arsenali ndo level za jangwani (Young Africa)
Mbona uwe fahari kwa wenzio michezo ya namna hiyo
Hatuikubali ni ya kidem
Ni sawa na kusema we ni mkali wakati sio
Na redio zinakupea promo hatari unauwa game
Asa kipi bora uwe na furaha na umekwazika
Ama uone kinyaa ati uwanja umetapika
Maana ina fahamika
Mziki nao mziki na mchwano ni mkali kati ya biashara na hailipi
Biashara imeshindwa la lahaula inang'ara
Wa mabingwa wanalindwa kama Paula Wakajala
Alafu wanatuweka roho juu kwa mikwala
Wakati tunajua hawakosi show tu wanakosa hadi pahali pa kulala
Wasanii uchwara, wasanii hawajala
Wasanii wana njaa wameshaweka duara
Wasanii mafukara, Bongo wasanii mikwara
Hao wasanii wametia kila kampuni hasara
Bongo noma regeza mjini Babu unachekwa
Uliza Roma kwani alifanyiwa nini baada ya kutekwa
(Well, well, well) hio ni siri ya kambi
Na kuto waheshimu wakubwa hio ni akili ya bangi
Ila akili ya Mange ni kufunguwa duka
Ila asili ya rangi nyeupe ni kuchafuka
Akili ya msomi ni kujijengea future
Ila akili ya mjinga ni kutaka vyote kwa pupa
Kwa hiyo anakosa vyote
Na siku ndo inavyokuwa show zangu natisha
Ila Izraeli ndo anaye ua
Mungu ndiye anaye jua, upi mwisho wa mimi
So ananipenda ananilinda yuko pamoja na mimi
Alafu mi najituma bwana, nasema mi najituma
Nipate kusimulia nikipata jukuu zangu
Mi ni msukuma bwana, nasema mi ni msukuma
Ndo kitu me najivunia usukuma fahari yangu
Japo nasikia, wanasema natoa ngoma hazibambi
... Cjai diss iwa na Mange
Nakula sana stori lakini sio eti kitambi
Sina shawty ati nitafte kadem ati nikala Nandy (alalalala)
Acheni shetani apite hoja zingine za kike
Mi mmoja kati wanofanya hiphop isikilizike
Kwa hiyo staki tungombane ya nini tuchoshane
Usibebe tango lote baby kaa vipi tukatiane
If you love me, love me and show me your feelings
And if you don't talk, you will die alone
Cz always machungu yanabaki kwa watawaliwa
And we need love revolution man
Hey greatest
It’s time to wake up and watch Young Killer Msodokiii!